Bayern wamwita Zidane achukue nafasi ya Tuchel
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani inatafuta mrithi wa Tuchel na sasa imeamua kumgeukia kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinadine Zidane, ambaye katika siku za karibuni ameripotiwa kutamani kurejea kwenye kazi yake ya kufundisha.
Zinedine Zidane aliondoka Real Madrid Juni 2021, tangu wakati huo amekuwa akiwindwa na timu kadhaa kama Juventus, PSG na kuliwahi pia kuwa na tetesi za yeye kuchukua kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa.
Hata hivyo kwa muda sasa tangu apumzike, kumekuwa na kusitasita kwa upande wake wa kukubali kurejea kwenye kazi hiyo.
Taarifa zinasema hivi karibuni Bayern Munich imewasiliana na wakala wa Zidane kumuelezea nia ya klabu hiyo kutaka huduma yake.