Bei mpya ya sukari kwenye mfungo wa ramadhani yatangazwa
Eric Buyanza
March 11, 2024
Share :
Wakati waumini wa dini ya kiislamu wanatarajia kuanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza bei elekezi ya sukari ili kuwapunguzia gharama wananchi.
Akitoa taarifa hiyo wilayani Mjini Unguja, Waziri wa Wizara Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban ametaja bei ni Sh. 2,650 kwa kilo moja kwa upande wa Unguja na Sh. 2,700 kwa kilo kwa upande wa Pemba.
Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi alilolitoa hivi karibuni katika ziara yake ya kutembelea wafanyabiashara na kusikiliza changamoto zao.
Katika ziara hiyo Dk. Mwinyi aliitaka Wizara ya Biashara kutoa bei elekezi ya kuuzia sukari baada ya serikali kuondoa gharama za kodi katika bidhaa hiyo, ili kupunguza makali ya maisha hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.