pmbet

Beki AS Roma alivyokikataa Kifo uwanjani

Sisti Herman

April 15, 2024
Share :

Jana wakati mchezo wa Serie A kati ya AS Roma na Udinese ukiendelea, dakika ya 76 beki wa AS Roma Evan Ndicka raia wa Ivory Coast alikaa chini baada ya kupata shambulio la moyo wakati akiendelea na mchezo kabla ya kupoteza fahamu kisha kuwahishwa hospitali kwa msaada wa dharura.

Masaa baada ya mchezo huo klabu ya AS Roma ilichapisha taarifa ya hali ya mchezaji huyo kutengamaa na sasa amerejea kwenye ufahamu wake wa kawaida.

Wataalamu mbalimbali wa Afya wamehusisha tukio hilo na la nyota mbalimbali ambao walifariki uwanjani moja kwa moja kama Mark Vivian Foe na wengineo, hivyo kitendo cha mchezaji huyo kukaa chini baada ya kuhisi utofauti kwenye afya yake kimesaidia ukubwa wa tatizo ambalo pengine lingechukua uhai wake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet