Beki mpya Man Utd apata majeraha
Sisti Herman
July 31, 2024
Share :
Ikiwa ni wiki 2 tu tangu kutambulishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United, beki wa kimataifa wa Ufaransa Leny Yoro ameripotiwa kupata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal yanaweyoweza kumuweka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa huku ikiwa zimesalia wiki 2 tu ligi kuu Uingereza kuanza.
Yoro aliumia dakika ya 35 ya mchezo kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu dhidi ya Arsenal uliochezwa nchini Marekani huku Arsenal wakishinda 2-1 kwenye dakika 90 za mchezo na Man Utd kushinda kwa mikwaju ya penalti.
Yoro ameitumikia Man Utd kwenye michezo miwili ya Pre-season hadi sasa inayoendelea nchini Marekani, dhidi ya Rangers na Arsenal.
Video juu ni beki huyo akionekana na majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji.