Beki wa Ihefu aitwa timu ya Taifa Nigeria
Sisti Herman
March 10, 2024
Share :
Beki wa Klabu ya Ihefu ya ligi kuu Tanzania bara, Benjamin Tanimu ameitwa kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria kitakachocheza mechi za Kimataifa za Kirafiki dhidi ya Ghana na Mali.
Kwa rekodi za hivi karibuni, Benjamin anakuwa Mchezaji wa kwanza anayecheza Ligi Kuu Tanzania Bara kujumuishwa kwenye Kikosi cha timu ya wanaume cha Nigeria.