Beki wa Kaizer auwa na watu wasiojulikana
Sisti Herman
April 4, 2024
Share :
Beki wa Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini , Luke Fleurs [24] amefariki Dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea usiku huu huku Johannesburg na kabla ya kufanyiwa tukio hilo vyanzo vinaarifu kuwa Luke alitekwa .
Fleurs alisajiliwa na Kaizer mwezi October 2023 na nia yake kubwa ilikuwa ni kushinda taji la PLS akiwa na Kaizer ndoto ambayo hajafanikiwa kuitimiza hadi mauti yanamkuta