Beki wa Man City akiri ku-date na rafiki wa mke wake na kuzaa mtoto mmoja
Sisti Herman
January 29, 2024
Share :
Beki wa pembeni wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester City Kyle Walker amekiri kumsaliti mkewe Annie Kilner kwa kuzaa mtoto wa kike kwa siri nje ya ndoa.
Kyle mwenye umri wa miaka 33 akiwa katika mahojiano na The Sun News siku ya Jumapili amekiri hayo baada ya kuchagua kuishi na rafiki wa mkewe ambaye amezaa naye mtoto.
Walker na Kilner walifunga ndoa miaka miwili iliyopita na wamebahatika kupata mtoto wa kiume.