pmbet

Beki wa Yanga Princess na Serengeti Girls atimkia Ulaya kucheza UEFA

Sisti Herman

July 23, 2024
Share :

Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania kwenye michuano kombe la dunia wanawake chini ya miaka 17 mwaka 2022 Noela Patrick Luhala ambaye pia alikuwa nahodha wa Yanga Princess msimu uliomalizika amejiunga na rasmi na timu ya Asa Tel Aviv ya ligi kuu Israel.

Noela mwenye umri wa miaka 18 alijiunga na Yanga misimu mitatu iliyopita akitokea Mapinduzi Queens ya Njombe na anajiunga na timu hiyo iliyomaliza nafasi ya 4 kwenye ligi ya wanawake Israel kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa Mwanaspoti.

Asa Tel Aviv ni mmoja ya klabu zenye uwezo mkubwa nchini Israel ambapo msimu wa 2019/20 iliwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) na kumaliza nafasi ya 3 kwenye msimamo wa kundi A.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet