pmbet

Bella kuanza kusaidia vijana wenye vipaji kupitia lebo yake

Eric Buyanza

February 24, 2024
Share :

Mwanamuziki Christian Bella anasema kupitia label yake ambayo iliwahi kufanya kazi na kusimama kwa muda, sasa imerudi tena hivyo anawaalika wasanii chipukizi wanaojiamini kuwa wana vipaji na uwezo wamtafute na atawapokea kwa ajili majaribio na wale atakaoridhika nao atawasaidia.

Kwa mujibu wa Bella ambaye anakaribia kufikisha miaka 20 kwenye biashara ya muziki Tanzania, anasema ni wakati sasa yeye kama kaka kusaidia vijana wenye vipaji ambao wamekuwa wakihitaji msaada wake.

"Vijana wengi sana wako mtaani wanajua kazi, kuna waimbaji wazuri, kuna waandishi wa mashairi wazuri....wapo wengi lakini sio kila msanii ana nafasi ya kuwapokea" anasema Bella.

Bella anasisitiza kuwa yeye kama mwanamuziki ndoto yake kubwa kwasasa ni kutengeneza vijana ambao siku moja ataweza kukaa na kujivunia kuwa flani na flani amewatengeneza yeye.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet