pmbet

Bellingham aiua Barca jioooni, Madrid wakishinda El Clasico

Sisti Herman

April 22, 2024
Share :

Klabu ya Real Madrid imeshinda mchezo wake wa 3 msimu huu dhidi ya watani zao klabu ya Barcelona kwenye "El Clasico" baada ya jana kuibamiza mabao 3-2 na kuendelea kujisimika kileleni mwa msimamo wa La Liga.

Kwenye mchezo huo mabao ya Barca yalifungwa na Andreas Christensen na Fermin Lopez huku yale ya Madrid yakifungwa na Vinicius Jr, Lucas Vazcuez na Jude Bellingham ambaye alifunga la ushindi dakika za jioni ikiwa ni mara yake ya pili msimu huu kufanya hivyo dhidi ya Barca.

Hadi sasa kwenye msimamo wa Ligi, Real Madrid wanaongoza wakiwa na alama 81 huku Barcelona wakifuatia wakiwa na alama 70, wakibakiza michezo 6 tu kumaliza msimu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet