Bellingham ashinda tuzo ya Golden Boy
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Usiku wa jana kiungo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa Uingereza Jude Bellingham alitwaa tuzo ya Golden Boy Award 2023 inayotolewa kwa mchezaji bora chipukizi chini ya miaka 21 wa kalenda ya mwaka.
"Niliweka jitihada zangu zote kupambana na kujijenga lakini kiukweli sifa zaidi nitazirudisha kwa Mr. Ancelotti (Carlo, kocha wa Real Madrid) ambaye ananipanga nafasi ambayo hunifanya kuwa huru zaidi kutimiza majukumu yangu ya kwenye mbinu za timu uwanjani, na sasa tunapaa, shukrani zaidi kwake" alisema Jude alipohojiwa na jarida la Tuttospot ambao ni waandaaji wa tuzo hizo zinazotolewa kwa wachezaji wanaocheza barani Ulaya ambazo mshindi wake hupatikana kwa kura za waandishi wa habari za michezo.
Bellingham, hadi sasa msimu huu tayari amefunga mabao 15 na kupuka 4 kwenye michezo 15 huku rekodi zikionyesha kuwa ndiye mchezaji mwenye mwanzo bora kitakwimu kwenye historia ya timu hiyo ya karne.