Bellingham awa 'MVP' La Liga
Sisti Herman
May 29, 2024
Share :
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Jude Bellingham usiku wa siku ya jana ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Uhispania (La Liga).
Kiungo huyo raia kwa Uingereza huu ukiwa ni msimu wake wa kwanza La Liga na Real Madrid amemaliza msimu akiwa na takwimu bora kama;
- Amecheza mechi 28
- Amefunga magoli 19
- Ametoa asisti 6
Pia kwenye msimu huu Bellingham tayari ametwa tuzo nyingi ndani ya muda mfupi;
🏅 Kopa Trophy as Best Talent.
🏅 La Liga Player of the Year.
🏅 Golden Boy Award.
Hata hivyo Bellingham hakuhudhuria hafla za tuzo hizo kwasababu timu yake ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund.