pmbet

Bellinmgham afurahia kutwaa taji lake la kwanza na timu bora duniani

Sisti Herman

January 15, 2024
Share :

Mara baada ya klabu ya Real Madrid kutwaa kombe la Spanish Super Cup kufuatia ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Barcelona katika dimba la KSU, Riyadh, Saudi Arabia, kiungo mshambuliaji bora zaidi kwasasa duniani Jude Bellinmgham amechapisha kwenye mitandao yake ya kijamii ujumbe wa furaha kutwaa taji lake la kwanza akiwa na timu hiyo ndani ya miezi michache tangu ajiunge nao.

 

“Kombe la kwanza nikiwa na klabu bora zaidi duniani” lilisomeka chapisho hilo la kiungo huyo raia wa uingereza ambaye jana alipika bao moja, kupitia ukurasa wa instagram.

Magoli ya Madrid kwenye mchezo huo yalifungwa na washambuliaji wawili hatari wa timu ya Taifa ya Brazil Vinicius Jr aliyefunga mabao matatu (dakika ya 7’ 10’ 39’) na Rodrygo (dakika ya 63’) huku bao pekee la kufutia machozi la Barcelona likifungwa na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski (dakika ya 33’) huku beki wa timu hiyo Ronald Araujo akila umeme (kadi nyekundu dakika ya 71’)

Real wametwaa kombe hilo kwa ya 13 kwenye historia ya soka la Uhispania moja nyuma ya Barcelona walioshinda mara 14.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet