Ben Pol afunguka za kumuheshimu Diamod Platnumz.
Joyce Shedrack
February 18, 2026
Share :
Mwanamuziki @iambenpol ameweka wazi sababu zinazomfanya amuheshimu sana staa wa muziki wa Bongo Fleva, @diamondplatnumz .
Akizungumza na @nicktozy , Ben Pol amesema moja ya sababu kubwa inayofanya amuheshimu msanii huyo ni ( resilience) ustahimilivu wa Diamond ndani ya tasnia ya muziki, akieleza kuwa licha ya changamoto mbalimbali, msanii huyo ameendelea kusimama imara na kufanya kazi kwa bidii.
Aidha, Ben Pol amesisitiza kuwa ( consistency ) mwendelezowa Diamond katika kutoa kazi bora na kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva ni jambo la kuigwa na wasanii wengine.
Amesema mafanikio ya Diamond ni matokeo ya nidhamu, juhudi na kujituma kwake katika kazi ya muziki.
Tembelea YouTube Channel Yetu Ya PMTV TWO Kutazama Muendelezo Mzima Wa Interview Hii





