Benchikha aondoka Simba, Mgunda na Matola warithi mikoba
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Taarifa kutoka chanzo kinachoaminika ndani klabu ya Simba zimethibitisha kuwa Kocha Abdelhak Benchikha na wasaidizi wake baada ya jana kuisaidia Simba kutwaa kombe la Muungano kwa kuifunga klabu ya Azam 1-0, rasmi sasa wameachana na timu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili ya mkataba uliokuwa umebaki, Benchikha alipewa nafasi hadi mwisho wa msimu ila ameouomba uongozi kuondoka.
Juma Mgunda Kocha mkuu wa muda Simba na msaidizi wake ni Seleman Matola, Michael Igendia anakuwa kocha wa viungo.
Kikosi hicho baada ya kurudi Dar Es Salaam kitaunganisha moja kwa moja Ruangwa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namungo FC, Kikosi kitasafiri na Kocha Mkuu wa muda Juma Mgunda pamoja na msaidizi wake Seleman Matola.