Benchikha awatema watano Simba
Sisti Herman
January 10, 2024
Share :
Taarifa za uhakika kutoka kwenye kambi ya Simba inayojiandaa na nusu fainali ya Mapinduzi Cup huko visiwani Zanzibar zinasema klabu hiyo imeachana na wachezaji wazawa watano (5) ambao haitoendelea nao na tayari imewaondoa kambini.
Waliotemwa ni Shaban Chilunda, Jimmyson Mwanuke, Nasoro Kapama, Mohamed Mussa na Feruzi huku pia ikisemekana kuwa orodha inaweza kuongezeka.