pmbet

Benchikha kama Zidane, aipiga chini Algeria kisa Simba

Sisti Herman

January 28, 2024
Share :

Shirikisho la Soka Algeria linapiga hesabu ndefu za kumsaka mtu wa kurithi nafasi ya kocha mkuu wa mabingwa wao wa Afrika wa 1990 na 2019 baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Djamel Belmadi kupoteza ajira baada ya kuishia makundi katika fainali za Afcon kule Ivory Coast, huku Benchikha akitajwa.

Inaelezwa kati ya makocha watatu wanaopigiwa hesabu na shirikisho hilo, yumo Benchikha ambaye ni raia wa nchi hiyo na wengine wawili wenye asili ya taifa hilo. Makocha wengine wanaotajwa sambamba na kocha huyo wa Simba ni; Jean Fernandez, pia yumo Rabah Madjer.

Mapema jaribio wa Algeria hao kumchukua Zineddine Zidane ambaye ana asili ya taifa hilo, liligonga mwamba baada ya kocha huyo wa zamani wa Real Madrid kugomea ofa hiyo. Zidane ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria akiwa na mafanikio makubwa ya kubeba Kombe la Dunia 1998 enzi akiwa mchezaji.

Licha ya Algeria kuonyesha nia ya kumtaka Benchikha inadaiwa amegoma kuiweka kichwani ofa hiyo na kutaka kuelekeza akili yake Simba, “Nadhani bado ni mapema sana kufikiria kuondoka hapa (Simba), kuna safari ambayo tumeianza kati yangu na klabu hii siku chache zilizopita haitakuwa sawasawa kuondoka kwa haraka.” alisema Benchika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet