pmbet

Bendera ya Tanzania kuanza kupeperuka kesho Olympic 2024 jijini Paris

Sisti Herman

July 28, 2024
Share :

Pamoja na kuwepo kwa mvua kubwa jioni ya juzi Ijumaa Julai 26, 2024, ufunguzi wa michezo ya Olympiki ya Majira ya Joto 2024 jijini Paris, Ufaransa, ulifana sana na mataifa yote 205 yalishiriki.

Team Tanzania nayo ilishiriki katika ufunguzi wa mashindano hayo ya 33, ambayo yanahusisha Jumla ya wanamichezo 10,714 watakaoshiriki katika aina 32 tofauti tofauti za michezo na michuano 329 katika muda wa siku 19 zijazo.

Safari hii sherehe hizo za ufunguzi zimefanyika kwenye mto Seine ambapo timu zote zilifanya paredi zikiwa katika maboti kabla ya kushushwa eneo rasmi la protokali za ufunguzi, mgeni rasmi akiwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Karata ya kwanza ya Tanzania itatupwa na mcheza Judo Andrew Thomas Mlugu ambaye ataingia Ulingoni Julai 29 (Saa 5 Asubuhi za Tanzania)

Mtanzania wa pili kushiriki atakuwa muogeleaji Collins Phillip Saliboko: Ataingia Bwawani Julai 30 – Mita 100 Freestyle (Saa 6:15 Mchana saa za TZ)

Mtanzania wa Tatu muogeleaji Sophia Anisa Latiff: Ataingia bwawani Agosti 3 – Mita 50 Freestyle (saa 6:00 Mchana saa za TZ)

Watanzania wa mwisho kushiriki watakuwa wakimbiaji Marathoni: ambao watawasili Julai 7, wakitokea kambini Arusha.

Safari hii mfumo wa michuano ya Marathon umebadilishwa, ambapo tofauti na ilivyozoeleka, wanaume ndio wataanza kukimbia na wanawake ndiyo watamalizia.

Hivyo basi wakimbiaji wetu wa Marathon wanawake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wamepangwa kushiriki mashindano hayo Agosti 11, 2024, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya Paris 2024 Olympics.

Wakimbiaji wetu wanaume, yaani nahodha Alphonce Felix Simbu - nahodha na Gabrield Gerald Geay watashindana Agosti 10, 2024 

C&P Issa michuzi 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet