pmbet

Benki watumia masaa 2 kuhesabu Bilioni 2 za tajiri akiwa anasubiria

Eric Buyanza

April 10, 2026
Share :

Mwaka 2021 huko kwenye mji wa Shanghai nchini China, tajiri mmoja aliamua kutoa benki pesa zake na kuzipeleka kwenye benki nyingine takriban Yuan milioni 5 (sawa na shilingi Bilioni mbili za kitanzania) kwa sababu ya kutoridhishwa na ujeuri na huduma mbaya aliyopokea kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo.

 

Tajiri huyo aliyejitambulisha kwa jina la "Sunwear" alionyesha kusikitishwa kwake na huduma duni kwa wateja huku akidai benki hiyo haijilewi na imekuwa na majibu na huduma mbaya kwake licha ya yeye kuhifadhi mamilioni ya pesa kwao.

 

Jambo ambalo liligeuka stori zaidi ni baada ya tajiri huyo kuwataka wafanyakazi wa benki hiyo kumuhesabia (kuhakiki) kwa uhakika hela zote alizotoa, kazi iliyowachukua masaa 2 wafanyakazi wa benki hiyo kukamilisha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet