Bernardo Silva kuitema Manchester City, anaitaka Barcelona
Eric Buyanza
April 24, 2024
Share :
Bernardo Silva amekuwa akihusishwa na kuhamia Barcelona mara kadhaa misimu iliyopita, lakini safari hii tetesi zinasema kiungo huyo wa kati wa Ureno ameamua kuondoka Manchester City ana nia ya kuhamia Barcelona.
Silva mwenye umri wa miaka 30 ni mmoja wa wachezaji bora kabisa wa safu ya kiungo duniani.