pmbet

Besigye apandwa hasira na kuzirai akiwa mahakamani

Eric Buyanza

July 30, 2026
Share :

Mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu nchini Uganda, Kizza Besigye, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, alizirai mahakamani wakati alipokuwa akipinga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa bila kuwa na mawakili.

 

Dkt. Besigye na watu wengine wawili wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga kuipindua serikali ya Uganda kinyume cha sheria.

Mara tu shahidi anayejulikana kama Andrew Wilson Orlando, ambaye anajieleza kama mtaalamu wa masuala ya usalama alipoanza kutoa ushahidi, Dkt. Besigye alipaza sauti kupinga jambo hilo kabla ya kuzirai.

 

“Kesi ilikuwa imeanza lakini Besigye na mwenzake Obedi Lutale hawajakubaliana na hilo suala wanasema hawana Wakili, walikuwa wanaomba tu muda ili wapate mawakili wengine.” Alisema Kennedy Okello, Msaidizi wa kisiasa wa Besigye.

Baada ya Dk Besigye kuzirai, shughuli za mahakama zilisimama na akapelekwa kwenye gari la wagonjwa ambalo liliondoka kwa kasi. Frank Baine ni msemaji wa Idara ya Magereza ya Uganda.

 

“Lilikuwa ni tatizo la kushindwa kudhibiti hasira. Alikasirika sana kutokana na yaliyokuwa yakijiri mahakamani, akapatwa na mshtuko na kuanguka, lakini tulimuwahisha kwenye hospitali ya Murchison Bay iliyo ndani ya gereza la Luzira” alisema Frank Baine, msemaji wa idara ya gereza Uganda.

 

Dkt. Besigye na washitakiwa wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya uhaini, huku serikali ikidai kuwa walifanya mikutano na pia kutafuta silaha za kisasa kupitia Andrew Wilson Orlando,raia wa Marekani ambaye pia alikua askari wa Uingereza kwa lengo la kumuua Rais Yoweri Museveni na kuipindua serikali yake.
Dkt. Besigye, anaipinga kesi hiyo, akiita ni mateso ya kisiasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet