pmbet

BET wamuomba radhi Usher Raymond

Sisti Herman

July 2, 2024
Share :

Waandaaji wa Tuzo za BET wamemuomba radhi mkali wa R&B Usher Raymond baada ya hotuba yake kutosikika kwa mashabiki walioko majumbani.

BET iliomba radhi kwa mshindi huyo mara nane wa Grammy siku ya jana Jumatatu Julai 1, ikieleza kuwa kutosikika kwa baadhi ya vipande vya hotuba hiyo kumetokana na matatizo ya kiufundi.

Aidha waandaaji hao walitoa shukrani zao kwa msanii huyo kwa kukubali kuhudhuria katika tukio hilo muhimu na kutoa hotuba fupi huku wakiwataarifu mashabiki ambao walikosa kusikia hotuba hiyo kuwa kwa sasa inapatikana katika majukwaa ya BET.

Utakumbuka Usher Raymond alishinda Tuzo ya BET 2024 katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa miondoko ya R&B kwa mara ya tano.

Tuzo hizo zilifanyika Jumapili Juni 30, katika Ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles huku Usher akiwapiku wasanii kama Chris Brown, Burna Boy, Drake, Fridayy, October London, Bryson Tiller na wengine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet