BIA KURUDI VIWANJANI EPL: Marufuku ya miaka 41 kuondolewa!
Eric Buyanza
September 24, 2026
Share :

Mabadiliko makubwa yanakaribia kushuhudiwa katika soka la Uingereza baada ya Waziri Mkuu Andy Burnham kuashiria uwezekano wa kuondoa marufuku ya miaka 41 inayozuia unywaji wa pombe majukwaani wakati mechi zikiendelea.
Marufuku hiyo, ambayo iliwekwa tangu mwaka 1985 ili kudhibiti fujo, inazuia unywaji wa pombe sehemu yoyote ambayo mtu anaweza kuona uwanja.
Burnham, ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Everton, ameitaja sheria hiyo kuwa ni "ubaguzi na upendeleo" dhidi ya mashabiki wa soka. Amesema kuwa hakuna haki kwa mashabiki wa soka kubaguliwa wakati mashabiki wa michezo mingine nchini humo kama vile kriketi na rugby wanaruhusiwa kufurahia vinywaji vyao wakiwa kwenye viti vyao. Ili kupima athari za mabadiliko hayo, Burnham amependekeza kuanzishwa kwa mpango wa majaribio (trials) kwenye baadhi ya viwanja
Hata hivyo, mpango huu umekumbana na ukuta mkali kutoka kwa Kitengo cha Polisi wa Soka nchini Uingereza (UKFPU), ambao wameonya kuwa uamuzi huo ni wa "kukurupuka na hatari sana". Polisi wanahoji kuwa soka lina historia ya kipekee ya vurugu na tabia za uhalifu ikilinganishwa na michezo mingine, na pombe imekuwa kichocheo kikubwa cha fujo hizo.





