Biashara Kariakoo sasa kufanywa masaa 24
Eric Buyanza
July 6, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo kuhakikisha kuwa biashara katika soko la Kariakoo zinafanyika saa 24 pindi ujenzi wa soko hilo utakapokamilika.
Aidha, Rais Samia amemuagiza Waziri Jafo afanye kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili kusimamia sekta ya biashara katika soko hilo.
Rais Dkt. Samia amemtaka Waziri Dkt. Jafo kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mazuri baina ya wafanyabiashara na Serikali kote nchini pamoja na kutatua kero zao, hali itakayopelekea Serikali kukusanya mapato stahiki na wafanyabiashara kunufaika na biashara zao.
Katika kuhakikisha raia wa kigeni hawajihusishi na biashara zinazopaswa kufanywa na wazawa, Rais Samia amemuelekeza Waziri Jafo kufuatilia utoaji wa leseni kwa wazawa na wageni ikiwa ni pamoja na kusaiili wafanyabiashara na kuwa na kanzidata yao.