pmbet

Bibi aacha urithi wa shilingi Bilioni 7 kwa paka na mbwa, akiwaacha watoto wake

Eric Buyanza

January 27, 2024
Share :

Mwanamke mmoja mzee nchini China ameamua kuacha urithi wa dola milioni 2.8 sawa na (shilingi Bilioni 7 za kibongo) kwa paka na mbwa wake badala ya kuwaachia watoto wake watatu.
 

Bibi huyo anasema paka na mbwa wake walikuwa karibu yake muda mwingi wakati anaumwa na walikuwa wakimsaidia.
 

Inaelezwa kuwa Bibi huyo, aliandika wosia wake wa kwanza miaka kadhaa iliyopita, akiwagawia watoto wake watatu mali zake zote, lakini alibadilisha mawazo hivi majuzi baada ya kutelekezwa na watoto hao.
 

Kwa mujibu wa taarifa Bibi anadai watoto wake hawakuwahi kumtembelea kumjulia hali na kumhudumia kwa njia yoyote wakati alipokuwa mgonjwa huku wakiwa wamekata masiliano nae kabisa...hivyo ameamua kuacha mali zake zote kwa viumbe hao ambao wamekuwa karibu naye.
 

Bibi huyo mwenye makazi yake jijini Shanghai tayari amebadilisha usia wake na amendika mwingine unaosema pesa zake zote zitumike kuwatunza wanyama hao baada ya kifo chake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet