pmbet

Bibi aanza shule ya msingi akiwa na miaka 92, asema kujifunza hakuna kikomo

Eric Buyanza

May 16, 2024
Share :

September mwaka jana (2023) vyombo mbalimbali vya habari nchini India viliripoti tukio la Bibi wa miaka 92 kuweza kutimiza ndoto yake ya kuweza kusoma na kuandika. 

Bibi huyo aliyefahamika kwa jina la Sameeran alijiunga na Shule ya Msingi ya Chawli na miezi sita baadae akaweza kusoma, kuandika na kuhesabu.

Sameeran aliyezaliwa miaka ya 1930 anasema alitamani kwenda shule baada ya kuona watoto wake na wajukuu wakienda.

"Niliwaona wajukuu zangu na watoto wao wakienda shule, na nilitamani kutaka kusoma nao," aliiambia NDTV, na kuongeza, "Kujifunza hakuna kikomo cha umri."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet