pmbet

Bibi harusi auawa kwa risasi siku ya harusi yake

Eric Buyanza

June 23, 2025
Share :

Bibi harusi ameuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akitoka kwenye sherehe ya harusi na mume wake mpya huko kwenye Kijiji cha Goult, Vaucluse nchini Ufaransa jana usiku.

Watu watatu akiwemo mtoto wa miaka 13 pia walijeruhiwa huku mshambuliaji mmoja nae akifariki katika majibizano ya risasi.

Taarifa zinasema wanaume wanne waliofunika nyuso zao walifika eneo hilo wakati sherehe imetamatika na kuanza kufyatua risasi hovyo.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati maharusi wakitoka katika ukumbi wa kijiji hicho wakiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka 13, na kukutana na washambuliaji hao.

Tukio hilo limehusishwa migogoro ya magenge ya dawa za kulevya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet