pmbet

Bibi wa miaka 74 aiba pesa Benki akitumia Bunduki

Eric Buyanza

April 27, 2024
Share :

Huko nchini Marekani Bibi wa miaka 74 amekamatwa na kushtakiwa baada ya kuiba kwenye benki moja kwa kutumia bunduki. 

Bibi huyo aliyefahamika kwa jina la Ann Mayers, alifanya uhalifu huo Aprili 19, anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa kutumia silaha pamoja na kuharibu ushahidi katika tukio lililotokea kwenye Kitongoji cha Fairfield, kaskazini mwa mji wa Cincinnati.

Ikiwa atapatikana na hatia, Mayers anaweza kufungwa jela hadi miaka 15. Polisi walimkamata Mayers nyumbani kwake Hamilton muda mfupi baada ya wizi huo, na bunduki iliyotumika ilikutwa kwenye gari lake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet