Biden aipa Ukraine ruhusa ya kutumia silaha zake kuitandika ya Urusi
Eric Buyanza
May 31, 2024
Share :
Rais wa Marekani Joe Biden ameipa Ukraine idhini ya muda kutumia silaha za Marekani kushambulia ndani ya Urusi kwa lengo la kutetea mji wa Kharkiv.
Maafisa wa Marekani waliozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, wamesisitiza kuwa sera ya Marekani inayoitaka Ukraine kutotumia makombora yake ya masafa marefu pamoja na zana nyingine kushambulia ndani ya Urusi bado haijabadilika.
Uamuzi huo wa Biden uliripotiwa kwanza na shirika la habari la Marekani, Politico.
Maafisa wa Ukraine, haswa Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskyy, wamekuwa wakilalamikia vizuizi vya kutotumia silaha za magharibi dhidi ya Urusi vinaviweka vikosi vya nchi hiyo katika hali ngumu wakati Urusi ikizidisha mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki la Kharkiv.
DW