pmbet

Biden apewa 'Thank You' aweka wazi sababu za kujiengua kugombea Urais.

Joyce Shedrack

July 25, 2024
Share :

Rais wa Marekani Joe Biden ameweka wazi sababu iliyofanya asitishe Kampeni yake ya kuwania Urais kwa Mwaka 2024 na kujondoa kwenye kinyang'anyiro hicho kuwa ni ili kuokoa demokrasia licha ya kuamini rekodi yake akiwa Rais ilistahili Awamu ya Pili

Rais Biden mwenye umri wa miaka 81 ametoa kauli hiyo wakati akihutubia Taifa la Marekani akiwa Ikulu ikiwa ni mara ya kwanza kujitokeza hadharani tangu alipotangaza kujitoa kugombea Urais wa Nchi hiyo Jumapili Julai 21, 2024.

 

Biden amesisitiza kwenye hotuba yake kuwa amekubali kuachia nafasi hiyo lakini analipenda sana Taifa lake.

 

 “Nimeamua njia bora zaidi ni kupisha Kizazi kingine, hiyo ndiyo njia bora ya kuunganisha Taifa letu ,Nimeamua kuondoka kwenye ofisi hii lakini nalipenda sana Taifa langu" Rais Biden.

 

Sambamba na hilo Biden ameendelea kumpigia chapuo Makamu wake wa Rais Kamala Harris na kusema ni mwanamke ni imara,anauzoefu, ana uwezo na amekuwa mshirika wake wa ajabu kwake na kiongozi bora kwa Taifa lake.

 

“Sasa maamuzi ni juu yenu watu wa Amerika ”ameongeza Rais huyo akiwaachia kazi raia wa nchi yake kufanya maamuzi ya kuchagua mtu sahihi atakayewafaa.

Wakati Rais Biden akitoa hotuba hiyo baadhi ya wananchi walionekana katika jiji la Washington, DC wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Thank You President Biden’ yenye maana ya Asante sana Rais Biden wakionekana kumshukuru Rais huyo anayemaliza muda wake.

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet