Biden atia saini sheria itakayowezesha kupigwa marufuku Tiktok
Eric Buyanza
April 25, 2024
Share :
Rais Joe Biden ametia saini muswada ambao utawezesha kupigwa marufuku kwa 'app' maarufu ya TikTok kutumika nchini Marekani.
Baraza la wawakilishi la Bunge la Marekani lilipitisha muswada huo Jumamosi, huku Baraza la Senet likiidhinisha muswada huo Jumanne usiku.
Chini ya sheria hiyo mpya, inampatia mmiliki wa TikTok kutoka China miezi 9 kuiuza kampuni hiyo kwa mmarekani la sivyo itapigwa marufuku nchini humo.