pmbet

Biden atumia maandiko ya Biblia kuwaaga wa Marekani.

Joyce Shedrack

January 20, 2025
Share :

Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden ameandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa muda wote aliokuwa madarakani yakiwa yamesalia masaa machache kuelekea kuapishwa kwa Rais mpya wa Taifa hilo Donald Trump.

Biden ambaye tangu siku ya jana aliwashukuru wa Marekani kwa ushirikiano waliompa kipindi chote akiwa madarakani baada ya kuhudhuria kanisani siku ya jana katika Jimbo la Carolina amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa X zamani Twitter akinukuu sehemu ya maandiko ya Biblia.

 

Kupitia Mtandao wake wa X  Biden ameandika “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa .”

 

“Baada ya miaka hii yote ya kuwatumikia watu wa Amerika sijamwona mwenye haki ameachwa”

 

“Nawapenda wote,endeleni kuilinda imani na Mungu awabariki wote”. ameandika Rais huyo wa Marekani.
‭‭
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet