Biden kuipandisha Kenya hadhi ya kuwa mshirika muhimu
Eric Buyanza
May 24, 2024
Share :
Rais wa Marekani Joe Biden amesema jana kuwa ataifanya Kenya kuwa mshirika mkuu asiye mwanachama wa jumuiya ya NATO.
Biden alitoa ahadi hiyo wakati alipomkaribisha Rais William Ruto kwa ziara ya kitaifa iliyolenga kukabiliana ushawishi wa Urusi na China barani Afrika.
Hatua hiyo itaifanya Kenya kuungana na mataifa mengine 16 yenye hadhi hiyo, yakiwemo Israel, Brazil na Ukraine, na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kijeshi la kidiplomasia, ingawa hakutakuwa na makubaliano rasmi ya usalama.
Biden pia aliishukuru Kenya kwa kukubali kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa nchini Haiti, ambako kwa miezi kadhaa magenge ya uhalifu yameliacha taifa hilo dogo la kwenye mzozo wa kisiasa.
DW