Bifu la Drake na Kendrick Lamar lamuibua Kanye West ampakulia minyama Kendrick.
Joyce Shedrack
February 4, 2025
Share :
Rapa maarufu wa Marekani Kanye West amefunguka kuhusu bifu kati ya mastaa wenzake ambao ni Kendrick Lamar na Drake huku akimpakulia minyama Kendrick Lamar akidai kuwa yupo juu zaidi.
Kanye amefunguka hayo wakati akiwa kwenye sherehe zilizofanyika baada ya ugawaji wa tuzo za Grammy Los Angeles nchini Marekani siku ya jana.
"Kwa sasa huwezi kamwe kumhesabu Steph Curry ukimlinganisha na Drake. Anaweza kuangusha pointi 200 kwenye wimbo mmoja,” alisema Kanye
Rapa huyo ambaye alizua gumzo pamoja na mke wake Bianca kwenye usiku wa tuzo ameweka wazi imani yake kwa Drake akisema kuwa ni rapa mkali na lazima atarudi kwenye nafasi yake ni suala la muda tu.
.