Bifu la Shamsa Ford na Rose Ndauka lapamba moto.
Joyce Shedrack
July 7, 2025
Share :
Imekuwa kama series ya ugomvi kati ya Muigizaji na mwanamuziki #RoseNdauka pamoja na rafiki yake #ShamsaFord wakirushiana maneno mara kwa mara mitandaoni.
Kiki, ukweli, wivu pamoja na ushauri hakuna kilichotambulika kwenye ugomvi wao uliopamba kasi baada ya Rose Ndauka kuachia ngoma yake ya kwanza 2021 ndipo Shamsa Ford alipomshauri na kusema kuwa :"Rose Ndauka anapenda kuimba sio kwamba hajui, anamuelekeo kidogo na muda utaongea zaidi ila kwangu mimi naona bado kabisa anisamehe kwa hili bora tuendelee kufanya 'movie', mpaka huu mwaka uishe tutaona mengi muziki tuwaachie wakina Maua Sama, Nandy na Rosa Ree" Shamsa Ford.
Ila pia baada ya #RoseNdauka kuachia EP yake ya #MajibuRahisi mwishoni mwa 2024 maneno yalikuwa mengi shamsa pia alifanikiwa kuongea yake akiongezea na ushauri alioutoa hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram jambo lililopelekea kumkwaza Rose na kumjibu kuwa "Ninaishi kwa mipango yangu na kumtanguliza Mungu"
Kama Shabiki wa Waigizaji nguli kabisa wa kike hapa Bongo unaona hizi ni kiki shamsa anafanya au anamsapoti rafiki yake kuzidi kupeleka kazi zake mjini??