pmbet

‘Bikira’ mjamzito wa miaka 19 adai alipewa mimba na ‘Nguvu za giza’

Eric Buyanza

April 20, 2024
Share :

Huko nchini Colombia binti mjamzito wa miaka 19 ambaye anadai hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yoyote toka azaliwe...anaweka wazi kuwa amepewa mimba hiyo na nguvu za giza.

Msichana huyo alizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii June mwaka 2023 baada ya kukiambia kituo cha televisheni (TV Malambo), kwamba anaamini alipewa mimba na nguvu isiyo ya kawaida. 

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa, alisema baada ya kuota ndoto za ajabu na kuhisi uwepo wa ajabu katika chumba chake, alianza kukosa hedhi na mama yake alipompeleka kwa daktari kwa uchunguzi ndipo alipogundua kuwa alikuwa mjamzito.

Msichana huyo alikiri kwamba hadithi yake hiyo ni ngumu kuiamini, lakini yeye mwenyewe haelewi jinsi alivyopata mimba hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet