pmbet

"Bila pointi 3 wananchi hawatanielewa" - Gamondi

Sisti Herman

February 2, 2024
Share :

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema licha ugumu wa ratiba kwao kiasi cha kukosa muda wa kutosha kupumzika baada ya mchezo uliopita dhidi ya Hausing kwenye ASFC na kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar anaamini hakuna matokeo tofauti yanayowafaa wananchi zaidi ya ushindi.

 

 “Hatukuwa na maandalizi makubwa kama mnavyojua tumecheza jumanne, tumesafiri siku moja na mazoezi ya mwisho ya mchezo huu, kwahiyo tupo tayari kwa mchezo” alianza kusema Gamondi.

 

“Mbinu tutakazoingia nazo ni zilezile, nadhani kila mmoja anajua ipi ni staili ya uchezaji ya Yanga, Yanga ni timu kubwa na nyakati zote inahitaji kushinda, tumekuja kwa malengo hayo hapa kubeba alama 3, tunajua sio rahisi kucheza ugenini, nao pia wanahitaji kushinda, lakini tumejipanga kupata alama 3” aliongeza Gamondi aliponukuliwa na PM Sports

 

Yanga watashuka dimba la Kaitaba mjini Bukoba leo kukabiliana na Kagera Sugar, mechi itacheza saa 10 jioni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet