Bilionea la Kiingereza kuinunua Man United
Eric Buyanza
December 26, 2023
Share :
Bilionea wa mmoja huko nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 71 anayefahamika kwa jina la Jim Ratcliffe amekubali kununua hisa asilimia 25 za Manchester United kwa takriban Dola Bilioni 1.3.
Taarifa hizi zinakuja linakuja miezi 13 baada ya wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer, kusema wanafikiria kuuza ili kutafuta mbinu mbadala. Familia hiyo ya Marekani ilinunua klabu hiyo kwa Pauni milioni 790 mwaka 2005.
United wamekuwa na kipindi kibaya kwa miaka ya hivi karibuni hawajashinda Ligi Kuu tangu 2013, huku mashabiki wakiandamana mara kadhaa kushinikiza kuondoka kwa familia ya Glazer ambao ndio wamiliki wa klabu kwa sasa.