Bilionea la miaka 92, lachumbia mama mrembo wa kirusi
Eric Buyanza
March 9, 2024
Share :
Bilionea wa kimarekani mwenye umri wa miaka 92, Rupert Murdoch, amemchumbia mpenzi wake ambaye wamekuwa wakionekana pamoja kwa miezi kadhaa sasa Elena Zhukova, mwenye umri wa miaka 67.
Inaelezwa kuwa Rupert kwasasa yuko kwenye maandalizi kabambe ya kumuoa mama huyo (mwanabiolojia mstaafu wa kirusi).
Murdoch mzaliwa wa Australia ambaye aliukana uraia wa nchi hiyo na kuchukua wa Marekani, ni tajiri anayemiliki vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa.