Bilionea Mulokozi anunua Helikopta, atua nayo Babati
Sisti Herman
December 18, 2024
Share :

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd yenye makazi yake Babati Mkoani Manyara David Mulokozi hii leo Disemba 18,2024 ameingia kwenye kalenda ya mwaka huu kwa kufanya tukio litakalo weka kumbukumbu kwa wakazi wa manyara baada ya kutua na Helikota yake mpya katika uwanja wa Tanzanite kwaraa mkoani manyara akiwa na familia yake.
Aidha, Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara.
Mmiiliki huyo wa Kampuni ya Vinywaji changamshi amenunua ndege hiyo aina ya helikopta kwa lengo la kusaidia kupanua biashara zake kwa kuwafikia wateja maeneo mbalimbali kwa haraka.





