pmbet

Bilionea wa India agharamia harusi za watu 50 na kuwalisha kwa mwaka mzima.

Joyce Shedrack

July 16, 2024
Share :

Tajiri namba moja barani Asia kutoka Nchini India Mukesh Ambani ambaye hivi karibuni alitikisa Duniani kutokana na harusi kubwa na ya kifahari ya  kijana wake Anant Ambani iliyohudhuriwa na mabilionea duniani kote kuzua gumzo,imefahamika kuwa kabla ya harusi hiyo ya kijana wake iliyogharimu zaidi ya Trilioni 1.9 aligharamia pia harusi za wachumba 50 ambao hakuwa na uwezo wa kufanya sherehe ya harusi Nchini India.

 

Harusi hiyo iliyofanyika katika moja ya majengo yake Jijini Mumbai ilihudhuriwa na watu 8000 wakiwemo ndugu jamaa na marafiki wa maharusi hao 50 pamoja na familia ya tajiri huyo mkubwa Nchini India, mke wake, watoto na wajukuu zake.

Ambani aligharamia kila kitu kwenye harusi hiyo ikiwemo mapambo ya maharusi kama pete,mkufu, mavazi na hereni za dhahabu ambapo kila mmoja alipokea zaidi ya milioni 3 kwa ajili ya manunuzi ya mapambo yake binafsi.

 

Tajiri huyo pia amejitolea kuwasaidia maharusi hao mahitaji ya muhimu kwa ajili ya kuanzia maisha kwa muda wa mwaka mmoja kama chakulaa,godoro,mitungi ya gesi na mahitaji mengi mengi ya muhimu. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet