Bilioni 217 mezani! Martinelli kuweka rekodi ya mauzo Arsenal
Eric Buyanza
August 24, 2026
Share :

Arsenal ipo kwenye mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji wake Gabriel Martinelli kwenda klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia kwa ada ambayo itavunja rekodi ya mauzo ya klabu hiyo.
Klabu hiyo inafanya mazungumzo na Al Hilal na inahitaji ilipwe ada ya uhamisho wa pauni milioni 60 (shilingi Bilioni 217.4 za kitanzania) ili kumuachia winga huyo wa Brazil.
Baada ya kukataa ofa ya kujiunga na Galatasaray ya Uturuki mapema mwezi huu, Martinelli ameripotiwa kufungua milango na kukubali uwezekano wa kuhamia Saudi Pro League.
Kama Biashara hii itafanikiwa kwa kiasi hicho, basi itakuwa mauzo ya juu zaidi ya kihistoria kwa Arsenal.





