Bilioni 286 Kujenga uwanja Arusha
Sisti Herman
March 19, 2024
Share :
Serikali kupitia Waziri wa Sanaa , tamaduni na Michezo imekamilisha hafla ya utiaji saini na Mkandarasi China Southwest Architectural Design and Research Institute Corp. Ltd kutoka nchini China kwaajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa jijini Arusha ambao utagharimu kiasi cha biliono 286 mpaka kukamilika kwake huku ukikadiriwa kubeba mashabiki zaidi ya 30,000.
Kwenye picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa (kushoto) akisaini Mkataba huo na Mkandarasi China Southwest Architectural Design and Research Institute Corp. Ltd atakayejenga Uwanja huo utakaokamilika mwaka 2025 ili taratibu za ukaguzi kwaajili ya kutumika katika AFCON ya Mwaka 2027.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 19, 2024 Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela na viongozi wengine wa Wizara hiyo.