Bilioni 9 kutolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Iyad Ag Ghaly
Eric Buyanza
June 5, 2026
Share :
Serikali ya kijeshi ya Mali imetangaza kitita cha dola milioni 3.5 (takriban Bilioni 9 za kitanzania) kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa au kuuawa kwa kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Sahel, Iyad Ag Ghaly.
Ghaly, kiongozi wa kundi la JNIM, anatajwa kuwa mtu anayesakwa zaidi katika eneo hilo kutokana na kuongoza kundi kubwa la wanajihadi linalopambana na tawala za kijeshi nchini humo na katika mataifa jirani.






