pmbet

Binadamu anayeshikilia rekodi ya kula mende wengi kwa dakika moja

Eric Buyanza

June 8, 2026
Share :

Ken Edwards, aliyezaliwa Derbyshire nchini Uingereza ndiye binadamu anayeshikilia Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kula mende wengi zaidi walio hai ndani ya dakika moja.

 

Mnamo tarehe 5 Machi 2001, aliweka rekodi hiyo ya kushangaza kwa kula mende 36 walio hai ndani ya sekunde 60 kwenye kipindi cha televisheni cha The Big Breakfast huko London.

 

Mende aliokula wanaitwa (Madagascan hissing cockroaches), ambao ni moja ya aina kubwa zaidi ya mende duniani, ambapo mmoja anaweza kukua hadi kufikia urefu wa inchi 3 (sentimita 7.6).

 

Edwards alieleza kuwa wakati unamla mende huyu, anatoa kemikali fulani ambayo "hufanya kwenye koo uhisi kama umepigwa dawa ya ganzi".

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet