pmbet

Binadamu mzee zaidi duniani afariki na umri wa miaka 116

Eric Buyanza

January 4, 2025
Share :

Bibi wa kijapani, aliyefahamika kama mtu mzee zaidi duniani na kitabu cha Guinness World Records, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.

Tomiko Itooka alifariki katika makazi ya wazee katika jiji la Ashiya, Mkoa wa Hyogo nchini Japan.

Alichukua rekodi ya mtu mzee zaidi duniani baada ya Maria Branyas Morera wa Uhispania kufariki Agosti 2024 akiwa na umri wa miaka 117.

Bi Itooka alizaliwa Mei 1908 (miaka sita kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia) na alithibitishwa kuwa mtu mzee zaidi duniani Septemba 2024 na kukakabidhiwa cheti rasmi na Guinness World Records.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet