Bingwa mapinduzi kunyakua Tsh 100m
Sisti Herman
December 26, 2023
Share :
Kamati ya Kombe la Mapinduzi 2024 imetangaza zawadi za washindi wa msimu huu kwa kuweka bayana bingwa ataondoka na kitita cha Shilingi milioni 100, huku wa pili akizoa akinyakua Tsh 70 milioni. Zawadi hiyo ni mara mbili na ile ya msimu uliopita ambapo bingwa alipata TSh 50 milioni, hii ni kutokana na ukubwa wa michuano hiyo ikiakisi Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbarouk Othman alisema mbali na fedha hizo zawadi nyingine pia zitakuwepo ikiwamo ya mchezaji bora, kipa bora na nyinginezo.