Binti aliyebakwa alipa kisasi kwa kumnyonga mbakaji
Eric Buyanza
May 9, 2026
Share :

Huko nchini Sweden binti wa miaka 15 aliripoti kuwa amebakwa. Polisi walimpuuza. Miezi kadhaa baadaye, mwanamume aliyetuhumiwa kumfanyia kitendo hicho cha kikatili alikutwa msituni akiwa amenyongwa.
Nasasa kutokana na uchunguzi binti huyo na kaka zake wanne wamekutwa na hatia ya kumuua dereva teksi mwenye umri wa miaka 26.
Iko hivi, baada ya polisi kupuuza taarifa yake kuwa amebakwa....binti huyo alipanga kulipa kisasi na hivyo alimualika mwanaume huyo (Dereva Taxi) wakutane jirani na hifadhi ya Uppsala kwa ajili ya mazungumzo huku akiwa tayari amewaandaa kaka zake.
Hata hivyo baada ya kufika kaka za binti huyo walimdaka wakamkaba na kumuua na kisha kuutundika mwili wake juu ya mti ili ionekane kuwa amejiua mwenyewe kwa kujinyonga.
Mkuu wa uchunguzi katika kituo cha polisi cha Uppsala alikiri hadharani kwamba walipaswa kuichukulia ripoti ya binti huyo kwa uzito na kwamba huenda mauaji hayo yangeweza kuzuilika.
Ndugu mkubwa alihukumiwa kifungo cha maisha. Wengine walipokea kati ya miaka mitatu na minne kwenye jela ya vijana wadogo.





