Binti ana haki ya kurithi mali ya mzazi hata kama ameolewa - Mahakama
Eric Buyanza
June 16, 2026
Share :

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamua kwamba mabinti wana haki sawa za kurithi mali ya mzazi kama vile watoto wa kiume, bila kujali kama ameolewa au la.
Uamuzi huo ulitokana na mzozo wa urithi ambapo baadhi ya wanafamilia walibishana kwamba mabinti walioolewa wanapaswa kupokea sehemu ndogo au kutopokea kabisa sehemu yoyote ya mali ya urithi.
Hata hivyo, mahakama ilitupilia mbali hoja hii, ikithibitisha kuwa ndoa haiathiri haki ya binti kurithi.
"Mashamba mengi nchini Kenya yanamilikiwa, yanaendelezwa, na kudhibitiwa kulingana na dhana kwamba mabinti 'tayari wamefaidika kwingineko' kupitia ndoa," Mahakama ilisema.
Mahakama iliongeza kwamba ahadi zisizo rasmi au za kusemwa kwa mdomo tu za ugawaji wa ardhi kwa watoto wa kiume hazifungamani kisheria ikiwa hakuna stakabadhi sahihi za kisheria zilizokamilika wakati mzazi anaaga dunia.
Muhimu zaidi, mahakama ilithibitisha tena kwamba chini ya Kifungu cha 38 cha Sheria ya Urithi, kikisomwa pamoja na Katiba, binti na kijana wa kiume wana haki sawa.
BBC





