pmbet

Binti mfalme wa Dubai aipiga chini ndoa yake kupitia Instagram

Eric Buyanza

July 18, 2024
Share :

Binti wa kifalme wa Dubai Sheikha Mahra Bint Mohammed Bin Rashid Al Maktoum,amefanya jambo la kushutua na kushangaza wengi baada ya kutangaza kumtaliki mumewe Mohammed Bin Rashid bin Mana Al Maktoum kwa kutumia ujumbe wa kikatili kabisa wa talaka tatu aliouandika kupitia Instagram.

Binti huyo wa mtawala wa Dubai mwenye umri wa miaka 30, kwenye chapisho lake hilo la Instagram aliandika hiviiii; 

“Mpendwa Mume wangu, kwa kuwa unashughulika na wenza wengine, ninatangaza talaka yetu. Ninakupa talaka, ninakupa talaka, na ninakupa talaka. Kila la kheri. Mke wako wa zamani," ujumbe huo ulisomeka kwenye ukurasa wae wa Instagram.

Hili limetokea miezi miwili tu baada ya wawili hawa kumkaribisha mtoto wao wa kwanza.

Picha zote za mume wa Sheikha Mahra zinaonekana kuwa zimefutwa kwenye akaunti yake. 

Na pia kwenye akaunti ya Sheikh Mana inaonyesha picha za mke wake zimefutwa.

Wawili hawa walioana Aprili 2023 katika sherehe ya kifahari.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet